KIUNGO wa Yanga, Haruna Niyonzima angependa kiungo Hamisi Thabiti acheze pembeni yake kwenye mzunguko wa pili na kusisitiza kuwa mchezaji huyo anajua.
Niyonzima alisema: “Kwa upande wa vijana waliopo Yanga, nikiwa mazoezini huwa nafurahishwa sana na Thabiti kutokana na staili yake ya kucheza. Anajua wapi kwa kupeleka mpira na kwa wakati gani apeleke mpira kwa mchezaji husika, hivyo nafikiri anahitaji muda mwingi kucheza ndani ya uwanja kuliko kuwa nje.”
“Kocha inabidi awape nafasi na vijana pia, wengi wao wako vizuri na muda utakapofika waweze kucheza na kuisaidia klabu ya Yanga,” alisema Niyonzima ambaye hivi karibuni alitwaa tuzo ya Mwanaspoti Bora wa Soka 2012/13.
Mchezaji huyo amemwomba kocha kuangalia uwezekano wa kutoa nafasi kwa vijana wengi wa Yanga mzunguko wa pili unaoanza Januari mwakani
No comments:
Post a Comment