Abdallah Kibadeni |
KOCHA wa Simba, Abdallah Kibadeni anaamini kasi ya Mbeya City katika Ligi Kuu Bara itapotea muda mfupi utakapoanza mzunguko wa pili wa ligi.
Hadi sasa Mbeya City inashika nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi huku ikiwa na pointi 27 baada ya kucheza mechi 13, kushinda saba na kutoka sare sita huku ikiwa haijapoteza hata mchezo mmoja
.
Yanga ndiyo inayoongoza ligi ikiwa na pointi 28 ikifuatiwa na Azam FC yenye pointi 27 kama Mbeya City lakini ikiwa na tofauti kubwa ya mabao ya kufunga na kufungwa.
“Unaiona Mbeya City sasa inafanya vizuri, tambua kwamba mwisho wake unakuja na kama unabisha utakuja kuniambia. Siasa za soka la nchi hii ndizo zitakaoizima timu hii inayokuja kwa kasi na hilo litathibitika mzunguko wa pili utakapoanza,”alisema Kibadeni bila kufafanua kiundani.
Kibadeni alisema kitu pekee kitakachoinusuru Mbeya City ni kuhakikisha wanabaki katika misingi yao na kuhakikisha wanafanya mazoezi ya maana wakati huu ambapo ligi imesimama kwa muda.
Mbeya City, timu iliyopanda daraja msimu huu sambamba na Ashanti United na Rhino Rangers, imetoka sare na Simba na Yanga huku ikiwa haijafungwa hata mechi moja kama ilivyo kwa Azam.
Timu hiyo inayofundishwa na Juma Mwambusi imejikuta ikijizolea mashabiki wengi inapocheza Uwanja wa Sokoine, Mbeya tofauti na Prisons ya jijini humo na hata inapocheza nje ya mkoa huo pia imekuwa ikipata
No comments:
Post a Comment