LONDON, ENGLAND
WAMERUDI tena na Wayne Rooney peke yake ndiye amewarudisha tena Manchester United katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu England hasa baada ya kutoa kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Arsenal juzi Jumapili usiku uwanjani Old Trafford.
Beki wa zamani wa Liverpool, Jamie Carragher, ambaye kwa sasa ni mchambuzi mahiri wa soka nchini Uingereza, amekiri kwamba kiwango cha Rooney mbele ya Arsenal kimeirudisha Manchester United katika mbio za ubingwa.
Rooney alipiga kona dakika ya 27 ambayo ilitumiwa vyema na patna wake uwanjani, Robin Van Persie na kumpa ushindi muhimu kocha, David Moyes, ambaye alianza mbio za msimu huu kwa kusuasusa.
“Rooney ndiye sababu kwa nini Manchester United kwa sasa ipo nyuma kwa pointi tano tu kutoka kileleni. Hii siyo Manchester United tuliyoizoea na kuna wachezaji wengi hawafanyi lolote, lakini Rooney ndiye aliyeibeba Man United pake yake na kuifikisha ilipofika,” alisema Carragher.
“Unaangalia ubora wa wachezaji wa timu pinzani kama Ozil na Ramsey, lakini Rooney analeta nguvu na akili. Ni mchezaji wa Ligi Kuu England hasa na ndio maana ni mchezaji wa hali ya juu katika ligi yetu na Manchester United.
“Tumeongea msimu huu kuhusu kombinesheni za uwanjani na washambuliaji bora na nadhani Man United ina baadhi ya washambuliaji bora Ligi Kuu England na Rooney ni bora katika timu yake. Kiwango chake leo (juzi Jumapili) kimeonyesha kuwa ni mchezaji bora kwa mbali sana. Watu wengi wanaongelea uhusiano wa wachezaji uliopo Liverpool (kati ya Sturridge na Suarez) au Manchester City (kati ya Negredo na Aguero), lakini Rooney na Van Persie ni bora sana.
“Arsene Wenger alisema kabla ya mechi kuwa anamwona Van Persie kama mchezaji wa Arsenal, nadhani labda Robin alisikia na ndio maana alishangilia sana bao lake tofauti na mechi iliyopita alipooonyesha heshima. Hapa ameonyesha kuwa ni Man United halisi
No comments:
Post a Comment