Monday, 4 November 2013

Hatua muhimu za kuwa mrembo





WIKI iliyopita tuliangalia sehemu ya kwanza ya makala inayohusu njia sahihi ya kuwa na mwonekano wa urembo. Katika makala ya leo tutaangalia njia nyingine.


Kitu kingine muhimu ambacho kinaweza kukuonyesha kuwa wewe ni mrembo au la ni namna unavyotunza meno yako.

Kama meno yako ni machafu au hayana weupe wa kutosha huwezi kujiita mrembo unatakiwa kutengeneza suala hilo. Kitu cha muhimu kwa utunzaji wa meno ni kuhakikisha angalau unapiga mswaki mara mbili kwa siku, hapa namaanisha asubuhi na jioni. Njia nyingine ya kuwa mrembo ni kufahamu namna ya kujipamba uso wako.

Unatakiwa ufahamu poda maalum kwa ajili ya ngozi yako, unapokwenda dukani kununua poda hakikisha unalinganisha ngozi yako na poda husika.
Tafuta ‘moisturizer’, ambayo ni nzuri, pendelea kutumia mascara, kama unapenda ‘lip stick’ basi pendelea kupaka ya pinki lakini ambayo haijaiva sana. Pendelea kufanya ‘scrub’ kwa ajili ya ngozi yako ya mwili mzima, fanya ‘scrub’ angalau mara moja kwa wiki, hiyo itasaidia kuondoa ngozi iliyokufa na kukufanya ung’ae.

Mazoezi pia ni njia nzuri ya kukufanya uonekane mrembo. Kama unajihusisha na mazoezi maana yake ni kwamba huwezi kuwa na uzito mkubwa.

Kitu kingine ni kupata usingizi wa kutosha, kama hulali vizuri uso wako utachoka mapema na wakati mwingine unaweza kupata mikunjo ya uzee mapema. Kula mlo kamili, hakikisha hukosi mboga za majani na matunda kila siku


No comments:

Post a Comment