Thursday, 10 October 2013

SOMA MAKALA YA KUSIMIMUA ;URAISI UNAPOMTESA DIWANI OLD TRAFORD

      
Kocha wa Man U kwa sasa David Moye kushoto huku kulia akiwa kocha
 mstaafu wa timu hiyo Sir Alex Ferguson
      
Katika maisha ya ukocha dani ya Mancheste United Sir alex Ferguson aliwahi kusema’Sometime in football you have to hold up and say yeah they are better than us’(Wakati mwingine katika mpira wa miguu unapashwa kunyanyua mikono yako juu na kusema wapinzani wetu walikuwa bora kuliko sisi)

Maneno haya haya kwa sasa yanajirudia kila wakati kaika mioyo ya mashabiki wa Manchester United na hata kwa kocha wao mpya David Moyes.
Macho ya mashabiki wa Man U kwa sasa wanaamini zipo timu bora kuliko wao,zipo zinatisha kama ilivyokuwa timu yao wakati wa Ferguson,Ferguson alikuwa ni kama mungu mtu pale Old Trafford sauti yake ni zaidi ya kiongozi wa jeshi lililo vitani,msimamo wake kwa waamuzi ulikuwa zaidi ya waislamu wenye itikadi kali.

Mashabiki walimwamini zaidi hata ya viongozi wa dini zao.
Maisha yanasogea na hata mambo yaliyopo yanasogea na kupita,nykati za Ferguson zimeshapita,lakini mashabiki wanaona kama zimepita haraka na ameondoka kipindi ambacho bado wanamhitaji lakini wanasahau Ferguson ni mwanadamu hata hata kama akirudi leo ipo siku ataondoka au ndo wanaona ni heri angeondoka baada ya miaka 10 ijayo hata kama akiiongoza Man U kwa kutumia rimoti control akiwa kwenye kiti cha kutembelea.

Au ndo wanaogopa fedhea za mashabiki wa Arsenal au maneno ya kashfa kutoka kwa Morinho au tambo za Man City,Maisha ya mpira ndivyo yanavyotaka hata kama wewe mshabiki hutaki,nani angejua Ac Milan ingekuja kuwa hii isiyotajwa hata katika timu tano zenye uwezo wa kutwaa ubingwa wa Uefa,nani angejua Liverpool katika uora wake ingejua kuwa hii ya kukosa hata top 4 kwa kipindi cha misimu mine mfululuzo.

Nani angejua Camerooni ingekuja kuwa ya kumbembeleza Et’oo kila siku ili aokoe jahazi la timu yake yake ya taifa.Yote hii ni kwa sababu ya maisha ya mpira yanabadilika,leo wewe ukiwa na matokeo bora katika timu yako na mwenzak akiwa na matokeo mabovu basi tambua ipo siku mambo yatabadilika yeye atapata matokeo bora na wewe kupata matokeo mabovu.

Kwa sasa bado ni mapema kusema Man U chini ya Moyes mambo yatakuwa mabaya katika kipindi hiki cha hiki cha mwanzo lakini wachambuzi wengi wa soka wanaona kuna mlima mrefu wa kupanda,wanaona kama Moyes ameruka hatua  kubwa na kwenda moja kwa moja Man U kutoka Everton,huku alipotoka timu ikishika nafasi ya 10 kwenye ligi hayo ndiyo maendeleo hata kama isiposhiriki kombe la Ueropa hakuna anaekuuliza kwake ni jambo la kawaida.

Lakini amekwenda timu inayohitaji makombe kila msimu,timu inayohitaji kushiriki Uefa Champions league tena sio kuishia hatua ya makundi bali kwenye timu nne za juu na hata kutwaa ubingwa.

Haya kufanywa na Moyes kwa wakati huu bado ni kama simulizi iliyo kwenye ndoto au maono kwa mashabiki wa soka hasa wa Manchester walionesha kutokumkubali mapema na hata kuandika kwenye mtandao wa kijamii wa twiter kumtaka Ferguson arejee kwenye timu yao,uongozi wa Manchester umeshanesha upo tayari kuvumilia wakati wa mpito utakaojitokeza,hali ya kuvumilia kupoteza michezo miwili na kutoka sare mmoja ndani ya michezo 7,

Sio takwimu nzuri kwa timu iliyozoea ubingwa kama Man U,swali jepesi la kujiuliza hapa,mashabiki wa Man U wapo tayari kusafii na timu hii katika barabara yenye milima na mabonde,timu iliyozea kuongozwa na mfalme vipi inapotawaliwa na diwani hapa ndipo ninaposema ‘Uraisi unapomtesa diwani Old Traford.’ 

No comments:

Post a Comment