Shamsa Ford |
BINTI mwenye mvuto kuanzia umbile hadi kwenye kazi zake za kwenye runinga, Shamsa Ford, amesema wasanii wengi nchini hawawataji wapenzi wao kwa kuwa wanao zaidi ya mmoja
.
Shamsa ameliambia Mwanaspoti kuwa japo kuna wasiopenda kutangaza uhusiano wao, lakini wengi wanaonyamazia kimya jambo hilo wana idadi kubwa ya wapenzi hivyo wanaogopa ‘kugonganisha magari’.
“Kila mtu ana staili yake ya maisha. Wapo ambao hawapendi kuweka mambo yao hadharani, lakini wengi wanafanya hivyo kuogopa ugomvi. Mtu anao wengi sasa akimwanika fulani itakuwa shughuli,’’ alisema.
“Ndiyo maana msanii anaishia kusema ‘sina mpenzi’ au ‘ninaye ila siwezi kumtaja’. Kweli kuna ambao wana wapenzi hadi sita, sasa atamtangaza yupi amwache yupi?
“Kwa wasichana siri ya hili ni kutafuta pesa, wanaume ni sifa ya kuendekeza ngono tu.
“Mimi nilimweka wazi mpenzi wangu ambaye ni mchumba na mume mtarajiwa, ndiyo maana ninaheshimika, sifuatwi na watu wenye nia ya kutaka mapenzi. Nimeiweka wazi jamii kwamba nina mtu wangu, hii ni heshima kwa mtoto wa kike.”
No comments:
Post a Comment