Friday, 4 October 2013

KIKOSI CHA SPAIN CHATAJWA,TORRES,CARZOLA NA SOLDADO WAACHWA!!


STRAIKA wa Tottenham Roberto Soldado, Santi Cazorla wa Arsenal na Fernando Torres wa Chelsea hawamo kwenye Kikosi cha Spain kwa ajili ya Mechi za Kundi I za kufudhu  Kombe la Dunia.
Wiki ujayo, Oktoba 11, Spain wanacheza na Belarus na kufuatia Mechi na Georgia, zote Mechi za Kundi I ambalo wako kileleni wakiwa na Pointi 14 sawa na France lakini wao wamecheza Mechi moja pungufu.
Kocha Vicente del Bosque amemrudisha tena Kikosini Juan Mata wa Chelsea na Alvaro Negredo wa Man City lakini Santi Cazorla amekosekana kwa kuwa ni Majeruhi akiuguza enka yake.
Beki Alberto Moreno wa ameitwa kwa mara ya kwanza.
Nae Soldado, ambae ana Goli 7 kwa Mechi 12 za Spain, ameachwa kwa vile David Villa wa Atletico Madrid amerudi Kikosini.
Vicente del Bosque ameeleza kuwa Fulbeki wa Chelsea, Cesar Azpilicueta, hayumo Kikosini kwa sababu hachezi Chelsea na ameeleza: “Juanfran anastahili nafasi. Lakini tunao Azpilicueta, Montoya na Carvajal lakini hawachezi. Juanfran anaichezea vizuri Atletico!”
Mbrazil Diego Costa hakuitwa kwasababu FIFA bado wanapitia Makaratasi yake ili kumhalalisha kuichezea Spain badala ya Brazil alikozaliwa.
KIKOSI KAMILI:
MAKIPA: Iker Casillas, José Manuel Reina, Víctor Valdés
MABEKI: Álvaro Arbeloa, Juanfran Torres, Gerard Piqué, Raúl Albiol, Sergio Ramos, Ignacio Monreal, Alberto Moreno.
VIUNGO: Sergio Busquets, Mario Suárez, Xavi Hernández, Andrés Iniesta, Koke, Francisco Alarcón "Isco",Pedro Rodríguez, Jesús Navas, Cesc Fábregas.
MASTRAIKA: Álvaro Negredo, Juan Manuel Mata, David Jiménez Silva, David Villa.

No comments:

Post a Comment