Mshamuliaji wa Yanga Jerry Tegete |
STEVEN Mapunda ‘Garrincha’ amedai ni aibu kwa wachezaji wa kigeni kuongoza msimamo wa ufungaji mabao kila mara na kuwafunika wazalendo kama Jerry Tegete, John Bocco ‘Adebayor’ na wenzao.
“Hata msimu huu kuna kila dalili kuwa mfungaji bora atatoka nje kwani dalili zimeanza kujionyesha,” alisema Garrincha na kuongeza kuwa hali hiyo inaonyesha kuwa klabu zina wachezaji wazuri kuliko timu ya Taifa jambo ambalo haliwezi kufanya Taifa Stars ikawa na kikosi cha ushindani.
Mfungaji Bora wa Ligi Kuu ya Vodacom mwaka 2012/2013 alikuwa mshambuliaji wa timu ya Azam, Kipre Tchetche raia wa Ivory Coast ambaye hadi ligi inahitimishwa alikuwa na mabao 17 wakati Amisi Tambwe wa Burundi anayeichezea Simba kwa sasa anaongoza kwa ufungaji akiwa na mabao manane.
“Huwezi kuwa na kikosi bora cha Taifa wakati wafungaji bora katika Ligi Kuu ni wachezaji kutoka nje,” alisema nguli huyo wa zamani wa Simba na kuongeza kuwa hilo ni tatizo na mjadala unahitajika.
“Kujituma hakuna, mtu analilia kucheza Simba au Yanga na anapoipata nafasi amejitahidi sana, atacheza msimu mmoja unaofuata anaachwa kiwango hakuna,” alisema na kuongeza kuwa hali hiyo inachangiwa na walio wengi kutokuwa na mazoezi binafsi.
No comments:
Post a Comment