Sunday, 8 September 2013

Wanamichezo watambua thamani


Gareth Bale
Gareth Bale


Thamani ya haki ya sura na hadhi ya mchezaji imefikia viwango vikubwa ikilinganishwa na enzi zile kabla ya dereva wa magari ya mbio za magari...
ya Langalanga Eddie Irvine kujinyakulia pauni 25,000 kutoka kituo cha Redio moja iliyotumia picha yake kutangazia biashara bila idhini yake mnamo mwaka 1999.



Enzi hizo picha za wanamichezo maarufu zilionekana kama mali ya umma.
Lakini michezo ilipozidi kua maarufu kote duniani, umuhimu wa hati miliki za michezo na wachezaji wake kama chombo cha kuuzia bidhaa na wahusika wenyewe kunufaika na taaluma yao.
Nyota wa michezo kama David Beckham, Cristiano Ronaldo, na sasa Gareth Bale wote wamefaidi mapato makubwa yanayoweza kupatikana kupitia masoko ya kuuza bidhaa kama chupi na viatu.
"wanamichezo wamegundua uwezekano walio nao wa kufaidi kupitia haki zao, anasema Nigel Currie wa kampuni ya mauzo ya vifaa vya michezo Brand Rapport.
"hati miliki inaweza kutegemea mtu binafsi na juhudi zake Bale.
"lililo bayana ni jina mfano kama Gareth Bale, na ikiwa jina lako lipo kwenye jezi ya mchezo wa soka, hapa unapatia hati miliki moja kwa moja."
Kijana kutoka Wales Bale mwenye umri wa miaka 24, aliyehamia klabu ya Real Madrid kwa kitita cha pauni milioni £85m, anatazamiwa kuunda mamilioni ya fedha kupitia hati miliki ingawa tayari asili mia 50 itahifadhiwa na klabu ya Uhispania.

No comments:

Post a Comment