Friday, 6 September 2013

OZIL;UA ZURI LENYE UDHAIFU

Ozil: I chose Arsenal because of world-class Wenger
Ozil
‘Ukijifahamu upo kwenye giza basi ni rahisi kujua giza la mwenzako’hivyo ni rahisi kumshinda mpinzani wako hata kama ana silaha kubwa kuliko wewe,maneno hayo yaliwahi kusemwa...
na mzungu mmoja anejulikana kwa jina la Carl Jung.Ozil alijijua yupo kwenye giza ndio maana ameweza kufahamu giza lililopo kwenye klabu ya Madrid.
Nani angeambia siku ya mwisho ya usajili Ozil atahama Madrid akubali tena atakwenda Arsenal iliyowataja Suarez ,Higuani,Rooney na Gustavo mwisho wa siku kuishia kuwakosa,inahitaji imani ya kidini zaidi au jicho la maono ndio unaweza ukaamni,hata baadhi ya wachezaji wa Real Madrid walitoa taarifa baaada ya kupata uhakika Ozil amehamia Arsenal walisema alituambia kuwa ataondoka lakini hatukuamini kwa sababu tulifikiri anatania.
Ozil alimuona kocha wa Real Madrid kwa sasa yupo katika giza nene la kutokumuona yeye ni mchezaji wa kipekee,aliona dalili ya Isco kupewa nafasi zaidi katka kipindi hichi cha mwanzo wa msimu angali ni mgeni kikosini wakati,yeye ni mzoefu wa kila kitu pale bernabeu,anajua ampe nani pasi anapokuwa katika eneo Fulani na ampe pasi ya aina gani.
Alizidi kufikiria mbali kama hapa mwanzo wa msimu nimeanza kukaa bench na kuingia kipindi cha pili basi siku zitakaposogea mbele na Isco kuzoea basi itanipelekea kukaa benchi na kuwa mtu wa kucheza kombe la mfalme.
   Mashabiki 20,000 walikusanyika kwenye uwanja wa Bernabeu siku ya utambulisho wa Bale,inawezekana sio kila aliekwenda pale alikuwa na lengo la kumuona Bale akikabithiwa jezi namba 11 na kumsikiliza akisema anafurahi kutimiza ndoto za kucheza Real Madrid,wengene walikuwa wanamuwaza Ozil ndio maana wakaona kama tukijifungia ndani huku tukiwa na huzuni haitasaidia,wakaamua kwenda uwanjani kufikisha ujumbe kwa rais wa Madrid Ferentino Perez na kubeba mabango yaliandikwa  ‘Usimuuze Ozil’
Mashabiki hao walikuwa wanampenda ozil naamini si kwa sababu ya upole wa sura yake bali kwa uwezo mkubwa akili za haraka kuhusu mpira anapokuwa eneo loote la uwanja na jinsi anavyoweza kumtengenezea mfungaji nafasi.muandishi mmoja wa Bbc inchini Spain ailkaririwa akisema kama kuna kiungo ambaye alikuwa anawaumiza kichwa Barcelona ni Ozil.
Unaweza ukajiuliza swali jepesi kwa nini iwe hivyo kwa Barcelona wakati wana Xavi,Iniesta na fabregas,lakini jibu linakuja kwa kipindi cha misimu mitatu iliyopita Ozil ametengeneza nafasi za magoli kuliko kiungo yeyoye barani ulaya kwa kutoa pasi za magoli 47 na kutengeneza nafasi 323 huku akicheza dakika 7324 na kupiga pasi 4334 hivyo kuwa na wastani wa kupiga pasi moja ndani ya dakika mbili kwa kila mchezo.
Raha iliyoje unapokuwa na mchezaji wa aina hii,unamfurahia si kwa mpira maridani tu bali hata kwa muonekano wake,baada ya kutangazwa kusajiliwa na Arsenal mauzo ya jezi yamengezeka katika mtandao wa klabu hiyo,hicho ndicho kinachowauma hicho kinachowauma mashabiki wanaipenda Madrid hasa wanapofikiria Ozil alikuwa ndie mpishi mkubwa wa Ronaldo ndio maana kwa sasa Ronaldo amefunga goli moja katika mechi tatu za la liga.
Watu walishindwa kuelewa Perez alifikiria nini kwa kumuuza Ozil,walishindwa wampe jina gani litakalomfaa,ni ngumu kuusemea moyo wa mtu lakini ni rahisi kutafakari matendo ya mtu,zaidi ya asilimia 66 ya masbabiki waliotoa maoni juu ya usajili wa Ozil alisema hawajafurahishwa na kitendo hicho.

Kama kuna kitu kikubwa Ozil alichotaka kutoka kwa watu wa Madrid ni upendo tena hasa kwa kocha carlo Ancelot,lakini baada ya kugundua mambo hayapo hivyo basi la kufanya ni kwenda sehemu muafaka na kuchagua kwenda kwa Wenger,Ozil alikaririwa akisema ameongea na kocha wa Arsenal hivyo yeye ndio alimfanya kwenda pale,amejiona kama ua zuri lakini lenye udahifu wa kuataka kuheshimiwa na kupewa nafasi ya kwanza katika kikosi tena majira haya ya wachezaji wanapokuwa vichaa kuhusu kombe la dunia litakalofanyika Brazil mwakani.    

No comments:

Post a Comment