Mesut Ozil |
Ozil anaendelea kueleza nilionesha kila upendo kwa klabu ya madrid na kujituma kwa kila aina na uwezo nilionao lakini niligundua wapo baathi ya watu katka timu hiyo hawakuwa na imani na mimi.Katika siku za wisho wa wiki nilitangaza sitapenda kuondoka katika klabu ya Real lakini niligungua kocha carlo Ancelot hana imani.Mimi ni mchezaji ninaetaka kuaminiwa ili niweze kucheza vizuri kila wakati na hicho ndicho nilichokihisi kipo Arsenal.
Nimeshaangalia mbele na kumuona kocha wa Arsenal,arsene Wenger ameonesha imani na mimi,kabla ya kuchukua maamuzi ya kuhamia kwenye klabu hiyo niliongea nae kupitia simu na kuniambia mipango yake dhidi yangu mimi,amenieleza mengi juu ya klabu inamikakati gani na usajili wangu.
Natafuta changamoto mpya itakayonifanya niwe na furaha nimeshasikia Arsenal ina mashabiki wa pekee wanaopenda wachezaji na timu yao kwa ujumla na wapo katika jiji lenye ushindani wa soka muda wote.
Wenger aameshaonesha imani kwangu na kwa sababu hiyo nitafika mbali sana kwa ajili yake,nitapata muendelezo mkubwa wa maisha yangu ya soka vizuri ndani ya Arsenal.
No comments:
Post a Comment