kiungo wa Chelsea wiliam |
Baada ya kufungwa magoli 2-1 na timu ya Basel katika mashindano ya ligi ya mabingwa,kocha wa Chelsea Jose Morinho amesema timu yake ulikosa ukakamavu hivyo kupelekea timu yake kupoteza pointi tatu muhimu...
Osca aliipatia goli la kuongoza dakika 1 kabla ya kwenda mapumziko lakini mambo yalibadilika katika kipindi cha pili baada ya Basel kusawazisha kupitia Mohamed Salah na Marco Streller kuifungia goli la pili na la ushindi.
Timu imekuwa kama Yai changa ambalo bado halijakomaa,kama ukilidondosha lazima liharibike hata kama utalidondosha katika mazingira mazuri.
Ukweli tulipoteza mchezo uliopita wa ligi dhidi ya Everton,jana tumepoteza na huzuni metawala katika mioyo yetu lakini kesho(leo) asubuhi tutakwenda mazoezini na kurekebisha makosa tuliyoyafanya katika mchezo huu.
Morinho alizidi kuzungumzia mchezo wa timu yake dhidi ya Basel,Nafikiri huu sio wakati wa kongelea perfomance ya mchezaji mmoja mmoja lakini wakati ukifika nitazungumzia hilo jambo la msingi ni kupata point katika michezo inayofuata na kumaliza katika nafasi mbili za juu za kundi ili tufuzu katika hatua inayofuata.
No comments:
Post a Comment