Friday, 20 September 2013

FEGURSON NA SAUTI INAYOPASUA MIOYO YA WAAMUZI


Mark-Halsey-2276821
Kocha mstaafu wa Mancheste United,Sir Alex Feguson kulia na
 kushoto ni mwamuzi mstaafu Mark Halsey 

Anaweza kuwa ameshastaafu, lakini aliyekuwa kocha wa Manchester United, Sir Alex Ferguson bado ana uzito na sasa amewaponza waamuzi..

Mmoja wao, Mark Halsey amedai kwamba ilikuwa kawaida kwao kuwasiliana na Fergie kwa ujumbe mfupi wa maandishi (SMS) na sasa wameonywa juu ya tabia hiyo isiyovumilika.
Halsey naye alistaafu kama fergie mwishoni mwa msimu uliopita, ambapo kauli yake imeshitua wadau wengi wa soka, ikizingatiwa kwamba Ferguson na Manchester walikuwa wakishutumiwa kwa kupata matokeo ya kushinda katika wakati na namna ya kushangaza.
Halsey anadai kwamba alipata kuwasiliana na Fergie binafsi katika suala zima la kuungana mkono.
Mwamuzi huyo aliandika pia juu ya utata uliotokea dhidi ya mwamuzi mwenzake, Mark Clattenburg aliyedaiwa kumbagua mchezaji wa Chelsea John Obi Mikel, na akadai kwamba aliwasiliana na Fergie pia ili kupata kuungwa mkono naye.
“Nilibeba jukumu hilo mwenyewe nikampigia simu Sir Alex na kumwomba kulizungumzia. Alikubali na kutumia mkutano wake wa Ijumaa na waandishi wa habari kusema hadharani kwamba Mark asingeweza kusema mambo ya kukashifu kama yaliyodaiwa na Mikel na Chelsea. Kwa jinsi mambo yalivyokuwa, kauli yake ilisaidia sana,” akasema mwamuzi huyo.
Hata hivyo, alikiri kwamba ilichukua muda mrefu kuweza kumshawishi Fergie kuwa upande wake na kisha walikuwa na uhusiano mzuri sana.
Mwamuzi huyo anadai kwamba licha ya uhusiano wake na Fergie, na pengine waamuzi wengine, haikumaanisha kwamba angependelewa bali alijua kwamba wakizidiwa ndiyo uhalisi wa mchezo.
“Wachezaji na makocha hawawezi kumheshimu mtu anayetoa maamuzi ya upendeleo au uonevu,” anasema Halsey.
Licha ya maneno ya mwamuzi huyo kudai kwamba hapakuwa na hila katika yote, taasisi ya waamuzi iliyopewa jukumu la kusimamia mechi za wachezaji wa kulipwa, ikiwa ni pamoja na Ligi Kuu ya England, imekerwa.
Imeeleza haja ya waamuzi kuzingatia maadili, ambapo katika tamko lililotolewa na msemaji wao, taasisi hiyo imesema ni muhimu kwa itifaki kuzingatia.
Imeeleza kwamba masuala ya kuangaliwa kwa makini ni pamoja na jinsi ya kuwasiliana na makocha na wacheaji na kuhakikisha kwamba uadilifu unazingatiwa

No comments:

Post a Comment