Tuesday, 24 September 2013

BOLT ASAINI MKATABA MPYA NA PUMA

Usain Bolt
Bingwa wa Dunia na Olympiki Usain Bolt amesaini upya mkataba wake na wadhamini wake wa kampuni ya vifaa vya michezo Puma mpaka baada ya michezo ijayo ya Olympiki ya mjini Rio de Janeiro mnamo mwaka 2016.

Mjamaica huyo mwenye umri wa miaka, 27, amekua akidhaminiwa na kampuni hiyo ya Ujerumani tangu mwaka 2003, na mara ya mwisho alisaini upya mkataba wake ilikua ni 2010 katika kile kilichoelezwa kua mkataba mkubwa kabisa wa kudhamini mwanariadha duniani.
Bolt amesema anajivunia kuendelea na ushirikiano wake na Puma "kwa miaka ijayo".
Hapo awali alidokeza huenda akastaafu baada ya michezo ya Olympiki ya mwaka 2016 Games, lakini hivi karibuni alisema huenda akaendelea kukimbia mwaka moja zaidi.
Bolt ameshinda nishani sita za dhahabu katika michezo ya Olympiki na nishani nane za dhahabu katika michuano ya ubingwa wa dunia mbali na kushikilia rekodi ya dunia ya sekunde 9.58 katika mbio za mita 100.
Mkurugenzi mkuu wa Puma Bjoern Gulden amesema kampuni yake imekua ikimdhamini Bolt tangu umri wa miaka 16.
Mbali na mkataba wake na Usain Bolt, Puma pia kwa muda mrefu imekua ikiidhamini timu ya riadha ya Jamaican.
Mkataba huu unaipa hadhi kubwa Puma inavyoendelea na ushindani dhidi ya wakinzani wake wakubwa Adidas na Nike

No comments:

Post a Comment