Sunday, 25 August 2013

Uchafu wakithiri katika jiji la Arusha

Baadhi ya uchafu uliozagaa katika soko la  kilombero jijini Arusha

Wafanyabiashara wa soko la Kilombero lililopo katika jiji la Arusha wameiomba manispaa ya soko hilo kuwawekea eneo maalumu kwa ajili ya kutupa taka zao ili kuweka mazingira katika hali ya usafi
hali itakayosabisha kuepuka magonjwa ya milipuko kama kipindupindu na homa za matumbo
.Hayo yamesemwa na baadhi ya Wafanyabiashara wa soko hilo walipokuwa wakiongea na mwandishi wetu mapema hii leo.


 Mmoja wa Wafanyabiashara hao aliejitambulisha kwa jina la Haji Saidi amesema uchafu umekuwa ukizagaa kila sehemu katika soko  hilo hali inayopelekea kuwa kero kwa Wafanyabiashara na wateja.
Mfanyabiashara mwinine katika soko hilo aliejitambulisha kwa jina la Bi.Salma uchafu umejaa katika eneo wanalotupia taka hivyo kusababisha uchafu kuzidi kuzagaa na wao kukosa sehemuya kutupa taka hivyo kusababisha mazingira hatarishi kwa ajili ya afya zao.
Hata hivyo juhudi za kuonana na msimamizi wa soko hilo bado zinaendelea,wamemalizia kwa kuiomba serikali iingilie kati suala hilo kwani limekuwa kero ya muda mrefu na viongozi wa eneo hilo wamelifumbia macho pamoja na kukusanya ushuru kil siku lakini wameshindwa kutatua tatizo hilo.  Uchafu wakithiri katika jiji la Arusha

No comments:

Post a Comment