Sunday, 25 August 2013

Tatizo la maji katika eneo Arusha


Baadhi ya viongozi wa serekali wakizingua mpango wa kuondoa tatizo la maji Tanzania.

Wakazi wa mji  wa Kwamorombo eneo la Olasiti jijini Arusha waimeilalamiia serskali ka ukosefu wa maji safi na salama kwa muda mrefu na kutopata sulisho la tatizo hilo hivyo kusababisha maradhi ya mara kwa mara kama homa ya matumbo na kuarisha.
Wakizungumza na mwandishi wa habari wa blog hii  wamesema,wamekuwa wakipato shida kubwa
kwa kukosa maji  safi na salama kwa ajili ya matumizi ya kila siku kwa ajili ya afya zao.
Mmoja wa wakazi wa eneo hilo aliyejitambulisha kwa jina la Salum amesema,maji yanatoka kwa wiki mara moja na hivyo kupelekea kupata shida ya maji kwa wakazi hao.Maji hayo yanafuatwa mbali  kutokana na uhaba wa miundombinu hasa mabomba ya kutoa maji.
Hata hivyo juhudi za kumtafuta mwenyekiti wa eneo hilo ziligonga mwamba baada ya kupata taarifa kuwa amekwenda safarini hivyo kuwaacha wakazi wa eneo hilo katika hali ya sintofahamu lini tatizo hilo litapatiw ufumbuzi.
Sambamba na hayo wanakijiji wa eneo hilo wameiomba serekali kuwanongezea mabomba yakutosha ili kurahisisha upatinaji wa maji safi na salama kwa ajili ya afya zao.

No comments:

Post a Comment