MAPEMA wiki iliyopita uvumi ulisambaa nchini England kwamba gazeti maarufu la The Sun lilikuwa mbioni kuchapisha stori ndefu iliyohusu kashfa ya ushoga ya mlinzi mmoja wa sasa wa kushoto wa timu ya taifa ya England.
Hata hivyo, Gazeti la The Sun la juzi Jumapili lilikanusha kutaka kuandika stori hiyo, lakini bado mlinzi wa kushoto wa England na Chelsea, Ashley Cole akawahi kukanusha kwamba alikuwa hahusiki na kashfa hiyo.
Cole ameimiliki nafasi ya ulinzi upande wa kushoto tangu Machi 2001 na ndiye mchezaji wa pembeni aliyecheza mechi nyingi zaidi katika kikosi cha timu ya taifa ya England.
Na kama kutakuwa na ukwlei wowote katika habari hiyo ni wazi kwamba hilo litakuwa pigo jingine kwa mchezaji huyo ambaye kwa sasa anahaha kupata namba hiyo hiyo aliyoitawala muda mrefu katika kikosi cha Chelsea na hivyo hiyo kuwa nuksi nyingine inayomuandama mchezaji huyo.
Mashabiki wengi waliamini kwamba Cole alikuwa anahusika na kashfa hiyo.
Mwingine aliyeonekana kuhisiwa katika kashfa hiyo ni mlinzi kinda, Luke Shaw ambaye ameanza kuichezea timu ya taifa ya England katika pambano la kirafiki dhidi ya Denmark Machi 8 mwaka huu. Hata hivyo wote wawili wametumia mitandao yao ya mawasiliano kukanusha uwepo wa habari hiyo.
Cole aliandika katika mtandao wake akisema ‘strictly chicks only’, akimaanisha anapenda wasichana tu, wakati Shaw aliandika kwa kusema ‘Si mimi’. Cole alikuwa katika ndoa na mwanamuziki maarufu wa Kundi la Girls Aloud, Cheryl Cole ambaye pia aliwahi kuwa jaji wa michuano ya kusaka vipaji ya X Factor lakini ndoa yao ikavunjika mwaka 2010 kutokana na kile kilichodaiwa kuwa Cole hakuwa mwaminifu katika ndoa hiyo.
Uvumi ulitanda Jumamosi usiku iliyopita katika mitandao ya kijamii kwamba The Sun la Jumapili lingemtaja mchezaji mmoja katika kikosi cha kocha Roy Hodgson ambaye anahusika na kashfa ya ushoga.
Kama gazeti hilo lingefanya hivyo, huyo angekuwa mchezaji wa kwanza katika historia ya timu ya taifa ya England kujitangaza kuwa shoga. Hata hivyo gazeti hilo lilikanusha waziwazi kwamba stori hiyo ilikuwa imepikwa na watu wasiojulikana.
Huo ni mwendelezo wa habari za ushoga zikuibuka katika vyombo vya habari vya Uingereza baada ya staa wa zamani wa timu ya taifa ya Ujerumani, Thomas Hitzlspelger kujitangaza kuwa shoga Januari mwaka huu.
Nyota huyo wa zamani wa Aston Villa, Everton na West Ham amekuwa mchezaji wa kwanza wa Ligi Kuu England katika mfumo mpya kujitangaza kuwa shoga.
No comments:
Post a Comment