Tuesday, 25 March 2014

JOHAN CRUYFF: "NEYMAR NDIO TATIZO FC BARCELONA"



Gwiji wa soka wa FC Barcelona Johan Cruyff anaamini kwamba Neymar ni tatizo kubwa ndani ya klabu ya Barca, hii ni kutokana na mshahara mkubwa usio na uhalisia wa uwezo wake.

Mshambuliaji huyo mwenye miaka 22 alijiunga na Barca akitokea Santos na kwa haraka akawa mmoja wa wachezaji wa Barca wanaolipwa mishahara mikubwa sana.
Johan Cruyff


Cruyff anahisi mshambuliaji huyo bado hajaonyesha ubora wake katika kiwango cha juu, ingawa, pia anahisi wachezaji wenzie watakuwa hawana furaha na mshahara anaolipwa Neymar.

"Tatizo la Barcelona ni Neymar," Cruyff alikaririwa na gazeti la El Mundo Deportivo.

"Ni mchezaji mzuri, hakuna mashaka juu ya hilo, lakini huwezi kumsajili mwenye miaka 21 na kumlipa fedha nyingi zaidi kuliko wachezaji walioshinda kila kitu. Hakuna aliye bora kihivyo katika umri huo.

"Pia Barcelona tayari wana mchezaji mkubwa zaidi duniani - Lionel Messi na mchezaji kinda wa miaka 21 hawezi kuwa nae sawa."

No comments:

Post a Comment