Thursday, 20 March 2014

GUARDIOLA AELEZA SIRI ILIYOMTOA BARCELONA



KOCHA, Pep Guardiola, amefichua kwamba kichapo kutoka kwa Chelsea kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya miaka miwili iliyopita ndicho kitu kilichomfanya afungashe virago vyake na kuiacha Barcelona. Kocha huyo wa Bayern Munich kwa sasa, aliondoka Barcelona baada ya misimu miwili ya mwisho ya upinzani mkali kutoka kwa Real Madrid iliyokuwa chini ya Jose Mourinho, lakini mwenyewe alisema kipigo cha Chelsea Ulaya ndicho kitu kilichochochea zaidi kuondoka Nou Camp.
“Tulikuwa wazuri zaidi yao kwenye mechi zote mbili, lakini tuliruhusu mabao ya kijinga kwenye mechi ya kwanza na hilo walilitumia kwenye mechi ya marudiano na kututupa nje,” alisema Guardiola.
“Niligundua kwamba nisingeweza kuinusuru tena timu na kuifanya icheze kwa kiwango cha juu.”
Guardiola alitangaza uamuzi wa kuiacha Barcelona muda mfupi tu baada ya timu hiyo kutupwa nje ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na Chelsea Aprili 2012.
Bao la dakika za mwishoni la Ramires, liliisaidia Chelsea kusonga kwa faida ya mabao ya ugenini huku Barcelona ikipoteza ubingwa wa Ligi Kuu Hispania kwa Real Madrid na kubakia na Kombe la Mfalme pekee ambalo ndilo lililokuwa la mwisho kwa Guardiola klabuni hapo.
Guardiola aliongoza Barcelona na kuwa hatari sana baada ya kutwaa mataji 14 katika kipindi cha miaka minne

No comments:

Post a Comment