Wednesday, 19 February 2014
FIFA YAZUNGUMZIA SUALA LA AFYA KOMBE LA DUNIA
WACHEZAJI wote watakaoshiriki
Fainali za Kombe la Dunia za
Mwaka huu huko Brazil
watapimwa ikiwa wanatumia
Madawa ambayo ni marufuku
kabla ya Fainali hizo kuanza hapo
Juni 12 kwa kumujibu wa Daktari
Mkuu wa FIFA, Jiri Dvorak.
FIFA wanataka Timu zote 32
zitakazoshiriki Fainali hizo za
Brazil kutuma Ratiba yao ya wapi
Timu zao zitakuwepo kabla Machi
1 kwao ili waweze kujua wakati
gani Wachezaji hao watapimwa.
Hata hivyo, Jiri Dvorak ameeleza
Wachezaji hao na Timu zao
hawatajua ni wakati gani Wapimaji
watatua Kambini mwao na
watahakikisha kuwa hakuna Timu
itakayokwepa kupimwa kabla ya
Mechi ya Ufunguzi kati ya Wenyeji
Brazil na Croatia hapo Juni 12.
Dvorak amesema: “Nina furaha
kuwa Watu wana wasiwasi udhibiti
wa Madawa Marufuku utaanza lini
kwa sababu hatutangaza. Tutakuja
wakati wowote, mahali popote!”
Aliongeza: “Kuanzia Machi 1,
tutaomba tujue Ratiba ya Timu
zitakuwa wapi. Na sisi Makao
Makuu tutaamua wakati gani
tutazifuata. Kwa kuweka wazi,
tutawapima Wachezaji wote si
chini ya mara moja kabla ya
Mechi ya Kwanza!”
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment