Monday 20 January 2014

RIYAMA;UIGIZAJI NI ZAWADI KWA MWANANGU




MWIGIZAJI wa filamu, Riyama Ally amedai kuwa filamu ya Faraja ni zawadi kwa mwanaye Fatma ambaye kwake ni kila kitu.
Akizungumza na Mwanaspoti, Riyama alisema kwamba anampenda sana Fatma kiasi kwamba akimwacha kwa muda kidogo tu anahisi kupoteza kitu kikubwa.
Riyama pia alisema kwamba huwa anapenda kutumia muda mwingi kucheza na mwanaye na asingependa alelewe na mtu mwingine zaidi yake.
“Nampenda sana Fatma hata nikiwa sehemu za kurekodi lazima awe na dada wa kazi pembeni ili akilia nimchukue na kumbembeleza, ninampenda na ananipenda kwangu ni faraja ya matatizo yote nikiwa naye sina ‘stress’,” alisema Riyama.
Msanii huyo alisema hayo baada ya baadhi ya rafiki zake kudai kuwa Riyama akiwa na Fatma naye hugeuka kama mtoto kwa kutumia muda mwingi kucheza naye.
Riyama aliongeza: “Kama usipompenda mwanao na kumfurahisha ni nani atampa upendo wa kweli? Hakuna zaidi yako wewe."

No comments:

Post a Comment