Kocha wa Newcastle United Alan Pardew ameomba msamaha kutokana na kuongea maneno yasiyo ya kimichezo kwa kocha wa Man City Manuel Pelegrin katika mchezo wa ligi dhidi ya Manchester City.
Mchezo huo ulimalizika kwa City kuibuka na ushindi wa magoli 2-0,kocha huyo aliongea maneno hayo baada ya mwamuzi wa mchezo kukataa goli lilifungwa na kiungo Tiote likiamuliwa kuwa ni offside.
Akiongea na mwandishi wa habari Pardew alisema"Nilisikia uchamuzi juu ya nilichozungumza naomba radhi kwa asilimia mia moja,
Katika moyo wa kocha lazima kuna aina ya maneno ninayopaswa kuzungumza,nimeshamuomba radhi naamini amenisamehe.
Pelegrin alionekena kukubaliana na mwamuzi kwa kukataa goli hilo lakini Pardew aliendelea kmponda kamisaha wa mchezo .
'Naamini ni jambo gumu kukosoa kila maamuzi ya mwamuzi alisema mmoja wa watu waliokuwa kwenye meza uya kamisaa
Najua walikuwa wanacheza nyumbani na wanaumuhimu wake hiyo ndo jambo la msingi lililomfanya Pardew kulalamika
Nae Pelegrini alikosoa uamuzi wa kutomtoa nje Mapou Yanga-Mbiwa baada ya kumchezea rafu Samir Nasri wakati alikuwa ameshaoneshwa kadi ya njano kpindi cha kwanza.
No comments:
Post a Comment