Tuesday, 17 December 2013

WAJERUMANI WA ARSENAL WAFICHUA JAMBO



MASTAA wa Kijerumani wanaokipiga Arsenal; Per Mertesacker na Lukas Podolski, wamefichua kwamba wakati mwingine wamekuwa wakikiuka masharti ya vyakula wanavyotakiwa kula waliyopewa na kocha wao, Arsene Wenger.
Wenger ametoa orodha ya vyakula anavyotaka nyota wake wote wale, lakini Wajerumani hao wamefichua kwenda kinyume cha maagizo.
Beki wa kati, Mertesacker na mshambuliaji Podolski, walisema wakati mwingine wamekuwa wakijifungia vyumbani na kula vyakula wanavyopenda kwa siri. Alisema wanafanya hivyo kwa kumtumia mpishi wa Kijerumani wa Arsenal.
Katika hatua nyingine, kiungo wa timu hiyo Mesut Ozil aliibuka na jipya baada ya kudai atapenda Brad Pitt acheze filamu ya maisha yake.

No comments:

Post a Comment