Thursday, 5 December 2013

Scholes asikitikia makinda England




WIJI la Manchester United, Paul Scholes, amesema wanasoka chipukizi nchini England wanaumizwa na wingi wa nyota wa kigeni kwenye Ligi Kuu England.
Scholes ambaye aliibukia Old Trafford mwanzoni mwa miaka ya tisini, anaamini wachezaji makinda wa taifa hilo hawapati nafasi ya kuonyesha ubora wao tangu wakiwa watoto tofauti na ilivyokuwa wakati wake kutokana na sasa klabu nyingi kusajili wachezaji wengi wa kigeni.
“Wakati sisi tulipoibukia, karibu wote tulikuwa wachezaji wa England. Kulikuwa na mmoja au wawili tu kutoka Ireland au Wales,” alisema Scholes.
“Lakini kwa sasa kuna mataifa saba au nane ya Ulaya wachezaji wake wanakuja na kuibukia kwenye shule za klabu hiyo, ukiacha wale wanaosajiliwa. Hili haliwezi kuwasaidia wachezaji Waingereza. Lazima kuwekwe sheria maalumu kwa sababu kama si sasa basi baadaye kutakuwa na madhara makubwa.”

No comments:

Post a Comment