Saturday, 14 December 2013

Rooney awaongoza wanasoka Waingereza wenye pesa ndefu

I'll just leave this here: Wayne Rooney, dressed in a similar hue to his car, parks his expensive Bentley in a Manchester side street


TIMU yake ya Manchester United inagaragara kwenye nafasi ya tisa katika msimamo wa Ligi Kuu England, lakini straika Wayne Rooney anashika namba moja kwa wanasoka raia wa Uingereza wanaotesa kwa utajiri katika ligi hiyo.
Kwenye orodha ya wanasoka 10 matajiri, mastaa Rio Ferdinand, Frank Lampard, John Terry na Steven Gerrard wameingia ndani ya tano bora, huku jina la staa wa West Ham United, Joe Cole likiwaduwaza wengi kutokana na kuwamo kwenye orodha hiyo.
Wazawa wengine wenye pesa za nguvu kwenye Ligi Kuu England ni Ashley Cole, Michael Carrick na Ashley Young, huku James Milner akiwa mchezaji mwenye umri mdogo zaidi mwenye pesa kwa kuwa na umri wa miaka 27.
Rooney anavyofunika
Akiwa na umri wa miaka 28, supastaa huyo wa England soka lake limemfanya kuingiza pesa za nguvu na kuwaacha kwa mbali Waingereza wenzake kwenye orodha hiyo.
Akiaminika kuwa na kipato kinachofikia Pauni 45 milioni, Rooney anapokea mshahara unaokadiriwa Pauni 250,000 kwa wiki na kumiliki mikataba minono ya kibiashara ukiwamo wa kampuni ya Nike.
Kitokana na kipato chake, Rooney anamzidi mtu anayeshika nafasi ya pili, Rio Ferdinand kwa tofauti ya Pauni 8 milioni kutokana na beki huyo wa kati wa Manchester United kumiliki Pauni 37 milioni.
Rio anavuna pesa kupitia mgahawa
Kwa wanasoka Waingereza wenye pesa na wanaoendelea kung’ara kwenye soka, Ferdinand anatajwa kuwa na kipato cha kinachofikia Pauni 37 milioni, ambazo amekipata kupitia mshahara wake anaolipwa Manchester United na biashara yake ya mgahawa pamoja na jarida.
Staa huyo anamiliki mgahawa wake unaoitwa Rosso uliopo jijini Manchester unamfanya apige pesa nyingi zaidi ukiweka kando kipato kingine anachokiingiza kutokana na jarida lake la #5.
Kuwekeza kwenye miradi ya biashara ni kitu kinachomfanya Rio kupiga pesa za maana licha ya sasa soka lake kuelekea ukingoni kutokana na kuwa na umri wa miaka 35.
Wakongwe wa Chelsea nao watesa
Kiungo Frank Lampard na mabeki John Terry na Ashley Cole wamo kwenye orodha ya wanasoka matajiri wazawa wanaotesa kwenye Ligi Kuu England wakiwa na kikosi cha Chelsea.
Lampard anashika nafasi ya tatu kwa kuwa na kipato kinachotajwa kuwa Pauni 31 milioni na Terry akiwa kwenye nafasi ya nne, lakini akiwa amefungana na nahodha wa sasa wa England na Liverpool, Steven Gerrard, kwa kuwa wote wanamiliki Pauni 29 milioni.
Ashley Cole yupo kwenye nafasi ya saba na utajiri wake unaotajwa kuwa Pauni 20 milioni, kipato ambacho kilipungua kutokana na madhara ya kutalikiana na aliyekuwa mkewe, mrembo Cheryl mwaka 2010.
Joe Cole, Carrick si haba
Staa wa West Ham yupo namba sita kwa kuwa na utajiri unaofikia Pauni 22 milioni. Cole anamiliki miradi yake binafsi ya kibiashara ikiwamo Joe Cole Promotions, inayomiliki mali kadhaa huko Caribbean na Dubai.
Alipokuwa kwenye kikosi cha Liverpool alikuwa akivuna Pauni 90,000 kwa wiki na klabu hiyo ililazimika kumlipa Pauni 3 milioni kama fidia wakati alipoondoka Anfield.
Jarida la Hello lilimlipa Joe Cole Pauni 2 milioni ili kupiga picha kwenye harusi yake na mrembo, Carly Zucker, mwaka 2009, lakini mwanasoka huyo alizitumia pesa hizo kutoa misaada ya hisani kwa ajili ya kusaidia jamii.
Kiungo aliye fundi wa Manchester United, Carrick akiwa majeruhi kwa sasa anamiliki Pauni 16 milioni na hivyo kuingia kwenye orodha akiwa mchezaji namba nane, huku Waingereza wengine Ashley Young na Milner wakifunga 10 bora kwa kuwa na utajiri wa Pauni 13 milioni. kila mmoja.

No comments:

Post a Comment