Sunday, 1 December 2013

KAKA AWASHA MOTO AC MILLAN

Kaka

Mario Balotelli alifunga frikiki kipindi cha pili na Kaka pia akafunga na kusaidia AC Milan wanaohangaika kupata ushindi wa 3-1 nyumbani kwa timu inayoshika mkia Serie A Catania Jumapili, na kuhitimisha wiki ya masaibu mengi kwa mabingwa hao mara saba wa Ulaya.

AS Roma waliokoa rekodi yao ya kutoshindwa pale Kevin Strootman alipofunga dakika ya mwisho na kuwapa sare ya 1-1 wakiwa Atalanta nao Inter Milan wakajipata pabaya walipofunga bao la dakika ya mwisho na kutoka sare ya 1-1 nyumbani dhidi ya Sampdoria.
Sare hiyo ya Roma ambayo ni ya nne mfululizo iliwaweka katika alama 34 sawa na viongozi Juventus, ambao watakuwa wenyeji wa Udinese katika mechi ya baadaye.
Ushindi wa kwanza wa Milan ugenini msimu huu katika Serie A ulifikisha kikomo mkimbio wao wa kutoshinda mechi tano ligini, ingawa walilazimika kutoka nyuma ili kuupata.
Catania walishangaza Milan pale Lucas Castro alipofunga kwa kombora lililogonga Daniel Bonera na kuingia dakika ya 13 lakini Riccardo Montolivo alikomboa dakika sita baadaye na kuwapa nafuu wageni hao wanaosumbuliwa na majeraha.
Balotelli alikosa mpira wa kichwa baada ya saa ya mchezo lakini akalipa dakika tatu baadaye kwa kuchapa frikiki safi ya chini ambayo ilipenya ukuta wa walinzi wa Catania na kuweka Milan kifua mbele.
Kaka aliwahakikishia ushindi alipochomoka upande wa kulia na akatuma kombora hadi juu ndani ya neti kwa kutumia guu la kulia kukiwa na dakika tisa zilizosalia za mchezo.
Catania walikuwa wameshuhudia Panagiotis Tachtsidis akifukuzwa uwanjani kwa kumchezea vibaya Balotelli ambaye muda mfupi baadaye alihusika kwenye mzozo mkali kati yake na Nicolas Spolli, akielekezea kidole chake Mwargentina huyo kwa hasira kabla ya kutulizwa na wachezaji wenzake.
Wachezaji hao wawili hawakuadhibiwa na Balotelli aliondolewa uwanjani muda mfupi baadaye.
Milan wamepitia wiki ngumu nje ya uwanja huku afisa mkuu mtendaji Adriano Galliani akitangaza kwa hamaki Ijumaa kwamba amejiuzulu baada ya kuwa katika klabu hiyo miaka 28. Jumamosi, alibadilisha uamuzi wake na akaamua kubaki, akigawana majukumu na rais wa klabu

No comments:

Post a Comment