MWIGIZAJI Aunty Ezekiel amesema kuwa skendo zake nyingi zinazovuma zimekuwa ni za kutengeneza na si matukio halisi yanayotokea katika maisha yake.
Akizungumza na Mwanaspoti, Aunty Ezekiel alisema katika maisha yake ya ustaa amekuwa akikumbana na skendo nyingi ambazo zinamfanya ashtuke kusikia matukio yanayomhusu asiyoyafahamu.
“Sina muda wa kukaa na kuanza kufikiria au kuumia kwa nini nimekumbwa na skendo. Ukweli ni kwamba asilimia 80 ya skendo zinazoelekezwa kwangu si za kweli,’’ alisema.
“Kuna ile hali ya umeonekana upo na fulani eneo fulani basi watu wanaunganisha matukio, hata siku moja sijawahi kukaa na kuumia kuhusu kitu hiki na haitawahi kutokea,” alisema kwa kujiamini.
Aunty Ezekiel ambaye ni mtoto wa mwanasoka mahiri wa zamani wa Simba na Taifa Stars, marehemu Ezekiel Greyson, aliyetamba miaka ya 1970 na 1980 mwanzoni kwa sasa yupo katika matengenezo ya filamu yake mpya ya ‘Mwajuma Nipe’.
No comments:
Post a Comment