Arsene Wenger |
Kocha wa Arsenal,Arsene Wenger amewataka wachezaji wa timu hiyo kuwa na njaa ya kutwaa kombe msimu huu ili kuondoa ukame wa vikombe ndani ya klabu hiyo.
Arsenal itasogea mpaka uwiano wa pointi 111 kama itashinda mchezo wao unaofuata dhidi ya Man U,mchezo utakaochezwa siku ya jumapili.Akiongea na shirika la utangazji la Uingereza la BBC Wenger alisema,,
"Ukweli ni kwamba kwa sasa tuo katika ubora wetu na tuna njaa ya kutaka jambo fulani ambalo tunalitaka,"
Arsenal ina pointi 25 kwa michezo 10 iliyocheza katika ligi ndani ya msimu huu,ikiwa ni tofauti ya point 5 kwa timu inayomfuatia ikiwa na pointi 20.Ikiwa na rekodi nzuri ya michezo ya ugenini kwa kutofungwa michezo 15 mfululizo.
Washika bunduki hao wa London hawajashinda tangu mwaka 2006,huku ukijumuisha mchezo wa kufungwa magoli 8-2 August 2011.
Mapema wiki hii Wyne Rooney alisema ni mapema kusema Arsenal inaweza kushinda ubingwa wa lii msimu huu hukukukiwa na rekodi ya timu hiyo kutofanya vizuri katika mzunguko wa pili wa ligi.
Huku kocha wa Man U,David Moyes akiongelea sala linalifanana na hilo akasema bado ni safari ndefu kusema nani bingwa.
"Mwisho wa msimu kila timu itacheza na timu nyingine mara mbili,hapo ndipo mambo yanapoamuliwa na kuwekwa bayana na hapo ndipo utakapofahamu ni ipi timu iliyobora" Moyes alisema
Wenger aliongeza kwa kusema
"Arsenal ina nafasi ya kushinda kombe la ligi kama timu yeyote katika ligi,ligi yetu ipo wazi,tumeanza ligi vizuri lakini jambo la kufurahisha na kubwa zaidi ni pale tutakapo maliza vizuri,
"Tutajaribu kufanya kila jambo ili tuweke wigo wa point 11 na wao,
Wenger pia alizungumzia rekodi ya timu toka mwezi wa 12
"Mara zote tumekuwa na muendelezo bora baada ya Christmas,alisema kwa sasa hilo ndilo ninaloweza kuongea lakini hakuna anaeweza kujua nini litakalo tokea siku zijazo,
"Tumefanya mabadiliko katika safu yetu ya ulinzi na hilo tumeliona katika michezo miwili iliyopita lakini bado kuna mambo mengi ya kufanya,
"Hatuwezi kuishia hapa na kupumzika na kusema tumeshapata kile tunakihitaji,
"Kwa sasa hatujashinda chochote hicho ndo kitu cha msimgi katika siku zijazo,
Wenger aliongezea katika safari ya kwenda Old Traford,na kusema,,
"Kuna uzuri fulani unaopatikana ndani yake,kucheza na Man U bila ya Alex Ferguson,Ferguson ni mshindani kila wakati,
"Yeye na mimi ndio tuliokuwa makocha wa muda mrefu ndani ya EpL kabla yeye hajastaafu,
Robin Van Persie anacheza sehemu ya tatu tangu aondoke kwenye timu yetu,
"Mshambuliaji huyo alifunga magoli 26 katika msimu wa kwanza,Wenge anaamini kocha wa Man U kipindi kile mholanzi Rene Meulenesteen ambae ameshastaafu alikuwa ni chanzo kikubwa kwa kumshawishi mshambuliaji huyo kujiunga na timu hiyo,
"Robin Van Persie alishahuriwa na kocha huyo kujiunga na Man U,Ni ukweli kuwa Van Persie aliniambia kuwa anataka kujiunga na Man U kwa sababu yake,na si kwamaba niliongea na Ferguson kuhusu kumuuza mshambuliai huyo".
No comments:
Post a Comment