STRAIKA wa zamani wa Simba, Danny Mrwanda baada ya kusikia Juma Kaseja amesaini kuichezea Yanga, amesema: “Haya sasa Kaseja kazi kwako kuwaonyesha wabaya wako kama unaweza.
”
Mrwanda ambaye kwa sasa anacheza soka la kulipwa katika Klabu ya Hoang Anh Gia Lai ya Vietnam, aliliambia Mwanaspoti kutoka Vietnam kwamba;”Naamini Simba walimuacha (Kaseja) kwa sababu za watu binafsi na si kwa utendaji wake wa kazi, kwa viongozi wengi wa Simba ni kawaida yao wanataka wawe na wachezaji watakaowapigia magoti kila wakati.
Kikubwa Kaseja anatakiwa awadhihirishie Watanzania akiwa na Yanga kwamba kutoichezea Simba tatizo halikuwa uwezo ila ni mizengwe tu, kwa sasa kazi imebaki kwake,’’ alisema.
“Ninavyomfamu Kaseja ni mchapakazi na anajituma hivyo ni imani yangu atapata nafasi.”
alisema Mrwanda aliyeibukia AFC ya Arusha kabla ya kutua Simba.
Baada ya kukaa nje ya uwanja kwa nusu msimu bila timu, Kaseja alikuwa akifanya mazoezi na Ndanda FC na Simba B kabla ya kusaini Yanga ambako anakutana na makipa aliokuwa nao Simba, Deo Munishi ‘Dida’ na Ali Mustapha ‘Barthez’
No comments:
Post a Comment