WINGA machachari wa Simba, Ramadhani Singano ‘Messi’ ambaye kuna uwezekano mkubwa Januari mwakani akawa chini ya kocha mpya, amewatuliza mashabiki wa timu hiyo na kuwaambia mambo mazuri yanakuja.
“Tumefanya vibaya mechi za mwishoni na kupoteza baadhi ya pointi na kuishia nafasi ya nne lakini mashabiki hawapaswi kukata tamaa na timu yao, waisapoti kwa nguvu zote kwani huko mbele lolote linaweza kutokea,” alisema mchezaji huyo ambaye timu yake imeishia nafasi ya nne.
“Naamini ubingwa tunaweza kuchukua, hizo timu nyingine zimetangulia tu na hata ukiangalia pointi tunakaribiana hivyo watakwama tu mahali na sisi tutarudi juu, Simba ni mfalme wa pori hakati tamaa anapotafuta nyama, tunakwenda kujipanga na kuangalia wapi tulikosea, tukirejea tutakuja na nguvu kubwa na tutahakikisha tunapambana na kila mpinzani wetu na kupata pointi tatu kila mechi,”alisema Messi.
Simba imemaliza mzunguko wa kwanza wa ligi ikiwa nafasi ya nne baada ya kucheza michezo 13, imeshinda sita, imetoa sare sita na imepoteza mchezo mmoja, imefunga mabao 26 na imefungwa 13.
No comments:
Post a Comment