Monday, 11 November 2013

MASHABIKI WA SIMBA WAENDELEZA UBABE KWA YANGA KWENYE NANI MTANI JEMBE

Mashabiki wa timu ya Yanga Shinyanga wakionyesha mbwembwe
 


Mashabiki wa Simba wameendelea kutangaza ubabe kwa mashabiki wa Yanga baada ya kuwashinda kwenye mechi za mashabiki hao zilizochezwa jana kwenye miji ya Shinyanga na Moshi kupitia bonanza la Nani Mtani Jembe, lililoandaliwa na Kilimanjaro Premium Lager ambapo pote Simba walishinda. Hata hivyo Yanga waliweza kujipoza huko Moshi kwa kupata ushindi mnono kwenye michezo ya kufukuza kuku, kupiga penati kwenye goli dogo na kupiga danadana.
Shinyanga bonanza lilianza mwendo wa saa 9 alasiri ukitangulia mchezo wa kufukuza kuku ulitangulia ambapo mashabiki wa Simba waliibuka washindi dhidi ya Yanga. Baada ya hapo ulifuata mchezo wa kukimbia ukiwa umevaa gunia ambapo Charles Shija wa Simba aliibuka kinara kwa mikimbio 2 dhidi ya 1 wa Yanga. Ulifuata mchezo wa kuvuta kamba wanaume ambapo pia Simba walishinda yanga 2-1.
 Baada ya mchezo huo kulifuata mechi kali sana kati ya mashabiki wa Simba wa soka wa mkoa wa Shinyanga na mashabiki wa soka wa Yanga, ambapo katika mechi hiyo simba walipata penati kipindi cha kwanza na mchezaji Iddi Mobi hakufanya ajizi na kukwamisha mpira wavuni. Mpaka mapumziko Simba 1 Yanga 0, kipindi cha pili Yanga walikuja juu ili wasawazishe lakini bahati haikuwa kwao na kujikuta wanapachikwa bao la pili lililofungwa na Kulwa Mobi. Baada ya bao hilo Yanga walikuja juu na dakika 8 kabla ya kipenga cha mwisho walipata penati iliyotiwa nyavuni na Amani Rashid.  hivyo mpaka filimbi ya mwisho Simba 2, Yanga 1.
Huko Moshi mashabiki wa Yanga walishinda mchezo wa kupiga dana dana na kupiga penati kwenye goli dogo, kufukuza kuku. Kwenye mchezo wa soka, mashabiki wa Simba walishinda kwa goli 2 – 1 na pia walishinda kuvuta kamba. Bonanza hilo lilipambwa na Malindi Band, Msanii maarufu wa bongo flava wa Moshi ajulikanae kama Majirani pamoja na wasanii wa kundi la Black Warriors.
Kupitia kampeni ya Nani Mtani Jembe, bia ya Kilimanjaro Premium Lager inayozidhamini timu za Simba ya Yanga imetenga kiasi cha shilingi milioni 100 na kisha kuzigawanya kwa timu hizo ambapo kila timu inazo shilingi milioni 50 ambazo zinashindaniwa na mashabiki wao.

Meneja wa Bia ya Kilimanjaro George Kavishe alisema kuwa mashabikiwa Simba na Yanga wanatakiwa kushindana kwa kushiriki kwenye kampeni hiyo ili kuhakikisha kuwa timu mojawapo inapata fedha nyingi zaidi ya timu nyingine.

Akielezea namna ya kushiriki, Kavishe alisema kuwa mpaka kila timu imetengewa shilingi milioni 50 na kuwa mshiriki wa shindano hilo la Nani Mtani Jembe ambaye ni shabiki wa Simba au Yanga anachotakiwa kufanya ni kununua bia ya Kilimanjaro ambayo kwenye kizibo chake kuna namba ya kushiriki.

Alisema baada ya shabiki kununua bia ya Kilimanjaro na kuona namba ya kwenye kizibo, anachotakiwa kufanya ni kuchukua simu yake ya kiganjani na kuandika ujumbe mfupi wa maneno akianza na jina la timu anayoshabikia kisha anaandika namba iliyo kwenye kizibo na kuituma kwenye namba 15440.

Alisema baada ya shabiki kutuma namba hiyo, atakuwa amepunguza shilingi 10,000 kutoka kwa timu pinzani yaani ikiwa shabiki aliyetuma ujumbe huo ni wa Simba atakuwa amefanikiwa kupunguza shilingi 10,000 kutoka kwenye fungu la Yanga na ikiwa shabiki ni wa Yanga pia atakuwa amepunguza shilingi 10,000 kutoka kwa Simba.

Kwa mujibu wa Kavishe matokeo ya uwiano wa fedha zinavyopungua kutoka Simba au Yanga yatangazwa kila siku hadi siku ya mwisho wa shindano hilo Desemba 14, mwaka huu.

No comments:

Post a Comment