Friday, 8 November 2013

MAKALA YA KUSISIMUA; FERGUSON NI ZAIDI YA OBAMA

Alex Ferguson
                       

Kuna watu kwenye hiii dunia wanaishi maisha ya kukumbukwa kila wakati,maisha yao yanadhamani kila mshale wa saa unaposogea tena yanazungumzwa katika kila kundi la watu wengi.Kuna watu ambao ni viongozi katika maisha yao ya sasa na hata wanapokufa wanabakia kuwa viongozi.

Mmoja ya watu hao ni Sir Alex Ferguson,uongozi wake ndani ya Man U hakuan mtu anaeza kuusahau,japo ameshastahafu lakini kila mmoja anaiona dhamani yake katika moyo wake.

Maisha anayoishi Ferguson inawezekana ni zaidi ya ndoto alizokuwa nazo toka akiwa anacheza katika barabara za Scotland miaka 65 iliyopita ni zaidi ya mawazo aliyowaza wakati akitua Man U miaka ya 1986.Inawezekana hata viongozi wa dini aliopo hawakuliona hili katika ulimwengu wa roho.
Kwa sasa Ferguson anaishi maisha anayoyataka,anachagua aende kwenye fukwe gani akapumzike yeye na mkewe,anachagua aende kwenye kiwanja gani akacheze gofu,yote yaha ni mapunziko ya mwili lakini akili yake na akaunti yake ya benk ikiwa bado inafanya kazi kwa kuingiza pesa za kila inchi kwa mauzo ya kitabu kinachooelezea historia ya maisha yake mwisho kuwa paundi na kuendeleza mamilioni ya pesa ndani ya akaunti yake.
Kila anachogusa kwa sasa ni pesa akienda kuchambua soka katika kituo Fulani cha television ni pesa,akifanya mahojiano na gazeti Fulani au kituo cha radio ni pesa inaingia.Kila mtu anatamani kuishi maisha anayoishi Ferguson kwa sasa labda angeomba kitu cha tofauti kimoja kwa kupunguziwa idadi ya miaka na kurejea kwenye ujana maji ya moto ili labda aende katika fukwe za Copacabana zilizopo Brazil na kula maisha pamoja na akina Cleopatra wa leo.
Wapo watu wanaojaribu kutengeneza maisha yao ya umaarufu kupitia mgongo wa Ferguson,wakati Ferguson anaeleza mambo yaliyopo kwenye kitabu chake,alizungumzia mgogoro uliowahi kutokea kati yake na Roy Keane lakini Keane alijibu na kusema ni uongo na angependa siku moja wakutane uso kwa uso mbele ya kituo cha television na ayaseme hayo mbele yake.
Sioni kama Ferguson anasababu ya kusema uongo katika karatasi zinazohesabika za kitabu hicho huku akibakisha mambo mengine katika moyo wake huku ikamini labada atayasema kwenye toleo la pili na la tatu katika mwendelezo wa kitabu hicho  ila ni kauli ya Roy keane ikijaribu kuipeleka dunia anapotaka yeye.
Sipati picha kipindi kimoja cha Television kitamlipa Ferguson kiasi gani cha paundi wakati akichambua timu ya England na nyingine kwenye kombe la dunia.Pesa inafuata mkondo,mkondo wa pesa alioutengeneza kipindi kilichopita ndio unafanya pesa zielekee kwake bila kutumia nguvu za mwili wake kwa sasa.
Katika hii dunia kuna watu wakifa wanakufa na uongozi wao,dunia inabaki ikimjua yeye ni kiongozi na shujaa wao kwa wakati wote.Lakini kwa upande wa maraisi anapostahafu uongozi wake unaishia kwenye karatasi za mkataba alizosaini wakati anaingia madarakani na wakati anatoka labda kwa wale waliojitolea maisha yao kwa ajili ya watu kama akina Mandela hichi ndicho kitakachotokea kwa rais wa U.S.A,Barack 

No comments:

Post a Comment