Tuesday, 12 November 2013

Kaseja: Yanga ndio saizi yangu


Juma Kaseja
KIPA mpya wa Yanga, Juma Kaseja amezungumza jambo ambalo hakuna shabiki yeyote wa Simba atakayependa kulisikia. Unajua amesemaje?
Amesaini Yanga miaka miwili kwavile ndio timu yenye ubora wa hadhi yake.
Kaseja alisaini kuichezea Yanga kwa mkataba wa miaka miwili huku akipewa kitita cha Sh 40 milioni Ijumaa iliyopita.
Lakini kipa huyo ameahidi kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na makipa wa Yanga, Ally Mustapha ‘Barthez’ na Deo Munishi ‘Dida’ ambao awali alikuwa nao Simba wakawa wanasugua benchi hata kwenye mechi za kirafiki.
Akizungumza na Mwanaspoti, Kaseja alisema: “Nimesaini Yanga kwa sababu ni timu kubwa na nimeona ndiyo ya kiwango changu na si klabu nyingine yoyote ile. Hakuna siri kuwa, hapa Tanzania timu kubwa zinazofanya vizuri na kulipa maslahi mazuri Yanga ni mojawapo, sidhani kama kuna mchezaji yeyote anayeweza kukataa ofa yao na kujiunga na timu nyingine za chini,”alifafanua Kaseja.
“Zipo timu nyingine zilinifuata lakini hazikuwa za kiwango changu ndiyo maana niliachana nazo,”alisema Kaseja lakini hakuzitaja kwa majina ingawa Mwanaspoti.
“Nipo Yanga sasa na nilikuwepo Yanga hapo nyuma, nafikiri wenyewe walifurahishwa na utendaji wangu wa kazi hapo nyuma na ndiyo maana walinifuata nifanye nao kazi kwa mara nyingine tena.
“Na kitu cha kwanza ninachowaomba wachezaji, viongozi na mashabiki wote wa Yanga, tuwe kitu kimoja na kikubwa wanipe ushirikiano na mimi nawaahidi nitajituma kadri ya uwezo wangu kushirikiana nao vizuri na kuifikisha Yanga mahali pazuri.”
Akizungumzia changamoto anapokwenda kukutana na walinda mlango wenzake, Barthez na Dida kipa huyo alisema; “Changamoto ni muhimu na hakuna mahali utakosa changamoto. Dida na Barthez, nimefanya nao kazi kwa kipindi kirefu huko nyuma, sioni kama kutakuwa na jipya lingine.
“Tutakapokuwa pamoja ndiyo itajulikana kila kitu lakini lengo ni kuifanya Yanga ifikie malengo wanayokusudia, tutafanya kazi nzuri,”alisisitiza Kaseja.
Mwenyekiti Kamati ya Usajili na Mashindano, Abdallah Bin Kleb alisema, wamemsajili Kaseja ili kuongeza nguvu kwenye kikosi chao na lengo ni kufanya vizuri soka la kimataifa kwani wao watashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika mwakani.
Katika hatua nyingine, Kocha wa Taifa Stars, Kim Poulsen amekiri kufurahishwa na kitendo cha Kaseja kusaini Yanga lakini akamwambia hatamuita kwenye kikosi chake

No comments:

Post a Comment