KIUNGO Michael Essien ameungana na wenzake katika kikosi cha Ghana kilichoweka kambi nchini Uturuki kujiangaa na mechi yao ya mwisho ya mchujo wa fainali za Kombe la Dunia ziidi ya Misri Jumanne ijayo.
Staa huyo wa Chelsea alitua Istanbul Jumanne iliyopita usiku baada ya kocha wa Black Stars Kwesi Appiah kumpa ruhusu ya kuchelewa kujiunga kufuatia mazishi ya baba yake mzazi.
Appiah sasa kikosi chake kimekamilika kwa ajili ya kufanya mazoezi ya nguvu kabla ya kwenda kuwavaa Misri kwao ambapo watakuwa na faida ya kuwa mbele kwa mabao 6-1.
Hali ya usalama Misri imeimarishwa na jambo hilo limeipa imani Ghana kucheza mechi hiyo muhimu.
“Siogopi wala kuihofia timu ya Misri ingawa nimekuwa na wasiwasi wa kucheza Misri kwa sababu ya hali ya usalama. Hatuna kitu cha kufanya juu ya hilo japo kwa sasa hali imeonekana kutulia.”
No comments:
Post a Comment