LONDON, ENGLAND
KOCHA Mkuu wa Arsenal, Arsene Wenger, amekanusha uwezekano wa kikosi chake kuathirika na kuporomoka kwenye msimamo wa Ligi Kuu England baada ya kutupwa nje ya michuano ya Kombe la Ligi na Chelsea juzi Jumanne.
Kocha huyo Mfaransa ameshuhudia kikosi chake kikipata vichapo mara mbili mfululizo kwenye Uwanja wa Emirates baada ya kukung’utwa na Borussia Dortmund kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya kabla ya Chelsea kwenye Kombe la Ligi.
Lakini, hilo halimfanyi Wenger kuamini kwamba Arsenal imeanza kuchoka na kwamba itashushwa kwenye msimamo wa Ligi Kuu.
“Tusifikie kwenye hitimisho haraka hivyo,” alisema Wenger. “Nadhani kama ukihesabu pointi tulizovuna tangu Januari Mosi ni nyingi kuliko timu nyingine zote. “Ninaamini, muda mrefu ujao tutashuhudia Arsenal ikicheza kwa kiwango bora kuliko mechi hizi mbili zilizopita. Ni kweli ni ngumu kuvumilia kwa hiki kilichotokea kwetu wiki iliyopita na sasa. Lakini, kubwa tutaendelea na msingi wa soka letu katika mechi zijazo na kuondoa makosa tuliyoyafanya.
No comments:
Post a Comment