Sunday, 27 October 2013

VETTEL ATANGAZWA MSHINDI WA LANGALANGA

Sebastien Vettel


Mbio za magari ya Langalanga yaliyofanyika mapema leo nchini India ambako Dereva wa Timu ya magari ya Red Bull Sebastien Vettel alitangazwa mshindi wa mbio za msimu huu 2013 ingawa bado kuna mashindano ya mbio kadhaa zilizosalia.

Mjerumani huyo mwenye umri wa miaka 26 aliendesha gari lake bila bughdha yoyote kufanikisha ushindi wake wa mara ya sita mfululizo msimu huu na kujitokeza kua dereva wa nne katika historia ya mashindano haya kufanya hivyo.
Baada ya mbio hizo Vettel alisema, nashindwa hata kusimulia, nimevuka msitari wa kumaliza mbio nikapoteza kauli. Najitahidi kutafuta maneno lakini nashindwa. Ni hadithi ya msimu wa neema tupu, timu nzima ina furaha isiyo kifani na fahari kuona watu hawa wakiwa na furaha kama hii.
Ushindi huu ni wa sita mfululizo na wa kumi kwa ujumla wa msimu mzuri kwake ambao unaweza kumsogeza karibu na rekodi inayoshikiliwa na Schumacher aliyeshinda jumla ya mbio 13 katika msimu mmoja.
Licha ya uwezo wake wa kushinda hata hivyo, Vettel ameshindwa kua na mvuto katika ushindi wake. Mfano ni ushindi wake huko Ubelgigi, Uingereza, Canada na Singapore ambako alizomewa na kwenye medani ya India alisimulia na jinsi kuzomewa huko kulivyomuathiri.
Amesema kua nilizomewa ingawa sikufanya kosa lolote na hilo liliniudhi kiasi lakini majibu nimeyatoa kwa ushindi uwanjani.
Endapo Vettel atashinda mbio tatu zilizosalia huko Abu Dhabi, Marekani na Brazil atafikia pia ushindi wa mara tisa wa Albert ASCARI wa mwaka 1952 na 1953.

Hata hivyo mpango mpya wa utaratibu utakaoanza mwaka 2014 kuendelea mbele ukihusisha mfumo mpya wa Ingini za magari pamoja na mfumo wa kuwezesha ingini ziongezewe nguvu --yanaweza kuzidisha ushindani wa mbio hizi.

No comments:

Post a Comment