Tuesday, 29 October 2013

SIBABAISHWI NA PENZI LA PESA;SHAMSA FORD

Shamsa Ford

MWIGIZAJI, Shamsa Ford amesema yeye ni miogoni mwa wasichana wachache waliobahatika kuchumbiwa, pia kuwa na uwezo wa kujiingizia kipato, hivyo hawababaikii wanaume wenye pesa.
“Mimi binafsi nipo kwenye uhusiano wangu madhubuti na ninaweza kusema sijawahi kupata hayo majaribu ya wanaume wasiojiheshimu, lakini nimewahi kukaa na kuwasikia wanachokisema waliopata majaribu hayo,” anasema Shamsa.
Aidha Shamsa amewatetea waigizaji wa kike kwa kusema kuwa si kweli kwamba wao ni wahuni kupitiliza bali wakati mwingine huwa hawataki ujinga ndiyo maana wengine huambua kuwachafulia majina.
“Tatizo wasanii pia tunapigwa vita na watu wengi, wengine wanatusingizia kwa mambo ambayo hatuyafanyi ili mradi tu watuchafue mbele ya jamii,” anasema Shamsha.

No comments:

Post a Comment