STAA wa filamu, Amanda, amesema uzuri wa kitu hauwezi kufichika kwa kufunikwa na takataka ndiyo maana hata akivaa magunia umbile lake zuri litaonekana.
Msanii huyo aliongeza kwamba hata kama ataamua kuvaa nguo za bei rahisi bado ukweli kuhusu umbile lake zuri utadhihirika tu.
Amanda alifafanua zaidi kwa kusema kwamba mapambo na mavazi ya gharama mwilini mwake ni nyongeza tu kwani umbile zuri alilojaliwa linaweza kuvutia hata akivaa magunia.
“Kila ninachovaa kinanipendeza, si kwa sababu mimi ndiye bingwa wa mitindo au ninajua sana fasheni, hii ni kutokana na uzuri wa asili niliojaliwa, namshukuru Mungu kwa hili,” anasema Amanda.
Alisema hawezi kujizuia kuvaa nguo anayotaka eti atawatega watu wakati ndivyo alivyozaliwa, kwani hata kwenye hizo nguo zinazoitwa za heshima bado humwonyesha umbo lake halisi.
No comments:
Post a Comment