Msanii wa kuigiza filamu Hemed Sulemani |
MWENYEWE hujiita Hemed ‘Pretty Huge Dude’ (PHD), akimaanisha kuwa mwanamume mwenye mwili mkubwa ulio na mvuto.
Akizungumza na Mwanaspoti, Hemed PHD anayefanya vizuri kwenye filamu za Bongo, amesema kwamba hawajui wanaomchukia kwani huziona habari zao mitandaoni tu ila anachojua ni kwamba watu hao wanampenda.
Hemed ambaye pia ni mwimbaji anasema si rahisi kukichukia kitu usichokijua, ndiyo maana anaamini watu wanaojifanya kumchukia ni watu wanaompenda isipokuwa mafanikio yake yanawakera.
“Wakati mwingine kitu ukikipenda sana kupita kiasi unaweza kubadili uamuzi na kuamua kukichukia, siwajui wanaonichukia ila nina hakika ni mashabiki wa kazi zangu,” anasema Hemed.
Aidha anasema anawapenda wote: “Ninawapenda wote, hata wale mashabiki zangu waliojivika vazi la chuki dhidi yangu, nawaambia ili waishi kwa amani, wakubali tu Hemed mkali na wanapenda kazi zake.
No comments:
Post a Comment