Monday, 21 October 2013

WENGER ATANIA JINSI KITABU CHA FERGUSON KITAKAVYOKUWA


Kocha wa Arsenal,Arsene Wenger amatania na kusem huenda Alex Feguson akaandika kufungwa kwa timu yake katika michezo yao walicheza katika mashindano mbalimbali.


Feguson anatarajiwa kutoa kitabu chake cha historia ya maisha yake kitakachotolewa mapema siku za usoni.akongea na waandishi wa habari katika mkutano wa kuelekea pambano la ligi ya mabingwa dhidi ya Dortmund,wenger alisema,

"Naogopa kuhusu mambo yasiyokuwa mazuri amabayo yalitokea katika maisha yangu mimi na yeye,lakni sijui nini kitakachoaandikwa katika kitabu hicho'

"Nafikiria ni jambo zuri kwa yeye kutoa kitabu

"Inawezekana hajapata muda mrefu wa kufikiria yote aliyofanya katika kazi yake ya ukocha,kwa sababu ni muda mchache kwa yeye kuacha kazi na kutoa kitabu

"Inawezekana akatoa kitabu kingine katika siku sijazo,kukawa na toleo la pili,toleo la tatu kukawa na maboresho ya kitabu cha kwanza

"Huwezi ukamzungumzia yeye kama yeye utamzungumzia yale aliyoyafanya ndani ya klabu".

No comments:

Post a Comment