Thursday, 24 October 2013

Wachezaji wa Rugby wabainika kutumia dawa za kujiongezea nguvu

Baadhi ya wachezaji wa mchezo wa Ragby wamebainika kutumia dawa za kujiongezea nguvu.
Baadhi ya wachezaji wa mchezo wa Ragby wamebainika kutumia
dawa za kujiongezea nguvu
Wachezaji watano wa klabu zinazoshiriki ligi kuu ya mchezo wa Rugby nchini Uingereza wamebainika kujihusisha na matumizi ya dawa za kuongeza nguvu.

Katika ripoti ya kila mwaka inayotolewa na Shirikisho la mchezo wa Rugby nchini Uingereza inayohusu mapambano dhidi ya matumizi ya dawa za kujiongezea nguvu na kubainisha kuwa wachezaji waliobainika wataadhibiwa kwa siri na kutozwa faini.
Vipimo hivyo vinafanyika chini ya Mpango wa shirikisho hilo baada ya mfululizo wa vipimo nje ya michuano.
Uamuzi wa kuchukua vipimo kwa wachezaji kumeanza mwaka 2009 baada ya miaka 4 baadaye ambapo wachezaji waliondolewa katika michuano baada ya kugundulika kutumia madawa ya kujiongezea nguvu.
Wachezaji waliobainika kupitia vipimo hivo watahifadhiwa bila kutajwa hadharani ikiwa hatawarudia tena vitendo hivyo.

No comments:

Post a Comment