Sunday, 25 August 2013

Mabingwa wa TASWA waoja joto ya jiwe


mchezaji waA.J.T.C Said Lazima akisiliziza
mawaidha ya mwalimu wakati wa mapumziko

Timu ya soka ya A.J.T.C Stars ambao ni mabingwa watetezi wa mashindano ya vyombo vya habari maarufu kama TASWA imelazwa magoli 2-1 katika mchezo wa kujipima nguvu dhidi ya timu ya askari wa FFU mkoani Arusha.

A.J.T.C Stars waliuanza mchezo huo kwa kasi na kujipatia bao la kwanza katika dakika ya 30 ya mchezo kupitia mshambuliaji hatari wa timu hiyo Jeremiah na kupelekea shangwe kwa mashabiki wao waliofurika uwanjani.
Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika timu A.J.T.C.  ilikuwa inaongoza kwa goli moja kwa bila.Timu ya FFU ilionesha uhai katika kipindi cha pili baada ya kufanya mabadiliko kwa kikosi chote na kuingia wachezaji wa akiba.



FFU walifanikiwa kusawazisha bao kufuatia kutokea piga nikupige katika lango la A.J.T.C Stars.wakati mashabiki wakiamini mchezo huo utamalizika wa sare ya bao moja kwa moja lakini timu ya FFU ilijipatia goli la pili na la ushindi katika dakika za majeruhi na kupeleka huzuni kwa mashabikiwa ya A.J.TC Stars.
Akizugumzia mchezo huo kocha wa A.J.T.C Stars Samwel Charles,amesema mchez ulikuwa mzuri na upinzaniwa hali ya juu lakini mwamuzi alikuwa na makosa madogo madogo yaloypelekea kufungwa bao la pili.

No comments:

Post a Comment